News

By December 3, 2025 No Comments

Serikali yetu ya kaunti, kwa kushirikiana na Taasisi ya Rasilimali za Dunia World Resources Institute inaandaa sera ya urejeshaji mandhari ili kukabiliana na uharibifu wa misitu na ardhi ambao umesababisha maporomoko ya ardhi na tope kwenye eneo la ukanda wa milimani.

‎Sera hii inalenga kudhibiti shughuli za kilimo na makazi, kukuza mazoea ya kilimo endelevu na kurejesha ukanda wa milimani.

‎Mambo muhimu yaliyomo kwenye sera hiyo ni Kudhibiti shughuli za kilimo kwa kupunguza shughuli za kilimo na ufugaji wa mifugo katika maeneo hatarishi.

‎Kuhamasisha mbinu za kilimo rafiki kwa mazingira kwa ajili ya mazoea ya kilimo endelevu.

‎Urejeshaji wa ukanda wa milimani kupitia upandaji miti na urekebishaji wa ardhi iliyoharibiwa.

‎Ushiriki wa jamii kuwashauri wananchi katika michakato ya kufanya maamuzi.

‎Mpango huu unatarajiwa kukuza uhifadhi wa mazingira katika kaunti ya Elgeyo Marakwet na kupunguza visababishi vya uharibifu wa ardhi ambao husababisha maporomoko ya ardhi na kuhatarisha maisha na mali.

Skip to content